• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

RC Wangabo Aipongeza TRA Rukwa Kwa Kuvuka Kiwango Cha Makusanyo.

Posted on: December 25th, 2020


Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameipongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Rukwa kwa kuvuka kiwango walichopangiwa kukusanya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 pamoja na nusu ya mwaka wa fedha 2020/2021 huku akitoa maagizo kwa Wakurugenzi ambao mapato yao ya ndani bado yanasuasua.

Mh. Wangabo amesema kuwa mapato yatokanayo na kodi na vyanzo vingine ndio yanayotegemewa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati nchini ikiwemo Reli ya Kisasa ya SGR, mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, Miundombinu ya barabara, Elimu, Afya, Maji na mengineyo na hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati na kuwasisitiza kila wanunuapo wadai risiti.

“Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Mkoa wa Rukwa ulipangiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 13.78 kupitia TRA Hata hivyo, tulifanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 14.56 sawa na 106% na mwaka wa fedha 2020/2021 kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba, 2020, Mkoa wa Rukwa ulipangiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 5.23. Hata hivyo, tumefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 5.61 sawa na 107%, Haya ni mafanikio mazuri, hivyo TRA iendelee kufanya bidii zaidi katika kazi yao ya ukusanyaji wa mapato.”

Aidha ametoa maagizo kwa wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo kuweka nguvu kubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani Pamoja na kudhibiti kikamilifu matumizi ya fedha za Halmshauri ili kuwaletea maendeleo wananchi kwa wakati na kwa kuzingatia bajeti na mipango yao.

“Kwa Mwaka huu wa Fedha wa 2020/21, Halmashauri za Mkoa wa Rukwa zilikisia kukusanya shilingi 9,487,289,000.00 Hata hivyo, Kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01 Julai, 2020 hadi tarehe 22 Disemba, 2020 Halmashauri zimekusanya kiasi cha shilingi 3,682,531,918.16 sawa na asilimia 38.8 ambapo zilipewa kukusanya angalau asilimia 50.” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika salamu zake za Krismasi na Mwaka Mpya wa 2021 kwa wananchi wa mkoa wa huo na kuongeza kuwa Katika kipindi cha kuanzia tarehe 1.7.2020 hadi 22.12.2020 Halmashauri ya Manispaa ya sumbawanga imekusanya asilimia 41.3, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imekusanya asilimia 40.6, Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo imekusanya asilimia 39.9 na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi imekusanya asilimia 33.8

Katika kipindi cha mwaka ujao wa 2021 Serikali ya Mkoa itajielekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi mbalimbali bila shuruti. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ni lazima sasa iwe rafiki wa mlipa kodi

















Kunja zote
Chapisha zoteKatika dirisha jipya







RC Wangabo aipongeza TRA Rukwa kwa kuvuka kiwango cha makusanyo















Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.