Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza maafisa Tarafa katika Halmashauri zote za mkoa huo kuwabaini kisha kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wote wa vijiji walioshindwa kuwasilisha fedha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni 911.5 na kuzitumia katika matumizi binafsi huku akiwaonya maafisa hao kuto tumia pikipiki walizokabidhiwa na serikali katika shuguli za bodaboda.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi vyombo vya usafiri wa piki piki kwa maafisa tarafa wote wa mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya mh .Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli aliyoitoa tarehe 4 June 2019 baada ya kukutana na maafisa hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
‘’ Ni imani yangu kuwa maafisa tarafa mtakapo kabidhiwa pikipiki hizi mtazitumia kuwasimamia maafisa watendaji wa kata na vijiji kwa karibu zaidi kwani wapo chini yenu kiuwajibikaji. Hakikisheni kuwa mapato yote wanayokusanya wanayapeleka benki. Bado baadhi yao sio waaminifu kabisa, wamekuwa wakichukua fedha za serikali na kuzitumia bila kuzipeleka Benki.’’ Alisema Wangabo.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za mfumo wa kukusanyia mapato kwa njia ya kielectroniki (Local government Revenue Colletion information system LGRCIS hadi tarehe 30 Aprili 2020, fedha ambazo bado ziko mikononi mwa wakusanya mapato katika halmashauri zote za mkoa wa Rukwa ni shilingi 911,511,525.00.
Katibu tawala mkoani humo Benadi Makali, amesema jumla ya piki piki 12 zimekabidhiwa.
‘’Mkoa wa Rukwa umepatiwa pikipiki 12 kwa tarafa zote ambazo zilikuwa hazina vitendea kazi hivyo ikiwa ni pamoja na Matai, Kasanga, Mwimbi, Mwazye, Mambwenkoswe, Itwelele , kipeta , Mtowisa, Chala, Kate, Namanyere na kwamba pikipiki hizo zimefanyiwa usajili ili kuwawezesha maafisa tarafa kutekeleza majukumu yao ya kila siku. ‘’Alisema Makali.
Mkoa wa Rukwa una vijiji 339 , kata 39 zahanati 201 na vituo vya afya 24 hivyo kutolewa kwa vifaa hivyo kutawarahisishia maafisa hao kufika kwenye maeneo hayo kwa wakati.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.