Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka maafisa uhamiaji pamoja na watumishi wengine katika maeneo yote ya mipaka inayopakana na nchi ya Tanzania, Kongo ,Burundi na Zambia kuacha tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka hiyo.
Mh. Wangabo ameyasema hayo alipotembelea katika mpaka wa Kasesha uliopo katika kata ya katete wilayani Kalambo na kwenye mpaka wa Kabwe kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani humo kwa lengo la kuanglia usalama wa maambukizi ya ugonjwa wa corona dhidi ya watu wanaoingia kupitia mipaka hiyo .
“Kwahiyo muwe makini sana, vitendo vya rushwa marufuku na kila jambo lichukuliwe kwa umuhimu na uzito mkubwa sana, kumbukeni kwamba kwenye mipaka ndipo mmebeba taifa”,alisisitiza wangabo.
Aidha, Mh. Wangabo ameutaka uongozi wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya udhibiti wa ugonjwa wa Corona kwa wenyeviti wa vijiji vyote vilivyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyika kwani imebainika kuwa mara kadhaa vijiji hivyo hutumika kama bandari zisizo rasmi kuingiza wageni wanaotoka katika nchi za Jamhuri ya Watu wa Kongo, Burundi pamoja na Zambia.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya kalambo Msongela Palela ,amesema kudhibitiwa kwa maeneo hayo kutasaidia kwa kiasi kikubwa watu kutoka nchi jirani kuingia kwa kufuata taratibu kwani katika maeneo hayo kuna mwingiliano mkubwa wa watu ambao hutoka katika nchi jirani ya Zambia na kuingia Tanzania .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.