Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo ameitaka wizara ya ujenzi ,uchukuzi na mawasilino kuharakisha ukarabati wa meli ya MV Liemba ambayo kwa muda mrefu imekuwa haifanyi kazi na hivyo kuwalazimu wananchi kutumia mitumbwi na boti kusafirisha mizigo yao hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.
Amesema wananchi wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutumia vyombo kama mitumbwi na boti ambavyo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na meli kubwa ya MV Liemba ambayo usalama wake ni wa uhakika muda na wakati wote.
Ameyasema hayo kupitia mahojiano maalmu na kituo hiki ,ambapo amesema endapo meli hiyo ikikamilika uchumi utaongezeka sambamba na kurahishwa kwa usafiri wa mizigo na wananchi.
“Nitoe wito kwa wizara husika hii meli ya MV Liemba nimeambiwa hapa kwamba ikipita kwenda Zambia inaitwa ‘Our Baby’ mtoto wetu, sasa huyu mtoto wetu anaulizwa yuko wapi, Zambia wanauliza, sasa Wizara husika twende haraka isimamie hili jambo, MV Liemba itengenezwe, ’’amesisitiza mkuu wa mkoa wa Rukwa JaoachimWangabo.
Hata hivyo Mamlaka ya Bandari hapa nchini inaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu ya bandari katika Mkoa wa Rukwa inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 .7 katika wilaya ya kalambo na Nkasi hivyo kukarabatiwa kwa meli hiyo kutaongeza kiwango cha ajira kwa wananchi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.