Mkuu wa mkoa wa Rukwa,Joachim Wangabo ametoa mwezi mmoja kwa wakuu wa wilaya wa mkoa huo wahakikishe shule zote za msingi na sekondari zinaanzisha klabu za wapinga Rushwa lengo ni kuwawezesha wanafunzi kuwa wadilifu na viongozi bora wa badaye.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt, Halfan Haule wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na rushwa walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na maafisa elimu mkoani humo,alisema lengo la serikali ni kutokomeza kabisa vitendo vya rushwa.
"kupitia hadhara hii ningependa kutoa wito kwa wakuu wa wilaya zote katika mkoa kuhakikisha kila shule ya sekondari na msingi katika wilaya husika inakuwa na klabu ya wapinga Rushwa na taarifa ya utekelezaji niipate kabla au ifikapo mwishoni mwa mwezi februari" alisema.
Alisema kuwa katibu tawala wa mkoa ahakikishe maelekezo haya yanawafikia wakuu wa wilaya kwa barua rasmi na nakala ya barua niione kwenye jalada.
Alisema ili watoto na vijana wawe viongozi bora na wadilifu ,ni lazima malezi yaanzie ngazi ya familia na kuendelezwa shuleni hasa shule za awali , msingi na sekondari.
Mkuu wa TAKUKURU mkoni humo,Hamza Mwenda, alisema Rushwa ni uozo wa kimaadili.
"maadili ni siraha muhimu katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na ukweli kwamba rushwa ni uozo wa kimaadili na maadili kwa maana ya mwenendo mwema hujengwa ndani ya mtu tangu anapozaliwa alisema Mwenda.
Hata hivyo mafunzo hayo yameshirikisha walimu walezi wa shule za msingi na sekondari pamoja na maafisa elimu katika shule zote za
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.