• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

RC Wangabo Aviagiza Vyombo Vya Dola Kumsaka Na Kumkamata Mkadarasi Anajenga Barabara Ya Mji Wa Matai.

Posted on: November 28th, 2019


MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameiagiza tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kumsaka na kumkamata mkandarasi wa kampuni ya Grand Tech LTD ya jijini Dar es salaam inayotengeneza barabara ya Lami yenye urefu wa kilometa mbili katika mji wa Matai wilayani Kalambo kwa tuhuma za kulipwa fedha zaidi ya nusu ya kazi kisha kuitelekeza.

Agizo hilo alilitoa jana katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao cha bodi hiyo alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliyelalamikia mkandarasi huyo kulipwa fedha kiasi cha shilingi milioni 544.2 sawa na asilimia 67 ya fedha yote ya mradi huo ambayo ni shilingi milioni 899.7 na kisha kuitelekeza kazi hiyo.

Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi huyo alipaswa kuwa ameisha kamilisha ujenzi wa kipande hicho cha barabara na kufikia Novemba 2 lakini bado na mpaka sasa yupo kwenye muda wa makato kutokana na kuchelewesha kazi hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa aliiagiza takukuru kufikia siku ya jumatatu wiki ijayo ni lazima mkandarasi huyo awe amefikishwa mkoani Rukwa kwaajili ya kuhojiwa ili kujua sababu za yeye kutotelekeza kazi hiyo pamoja na mchakato wa kumlipa fedha zote hizo wakati kazi hiyo haina thamani ya kulipwa fedha hizo.

Kwaupande wake mkuu wa Takukuru mkoa wa Rukwa Hamza Mwenda aliahidi kutekeleza agizo hilo ili kuwaondolea kero wananchi wa mji wa Matai ambao wamekuwa wakilalamikia kipande hicho cha barabara kwakuwa kimekuwa kero kwakua ndicho kinacho chepuka na kuingia makao makuu ya wilaya hiyo kutoka katika barabara kuu ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda katika bandari ya Kasanga.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.