• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

RC Wangabo Awaonya Ving’ang’anizi Wa Madaraka Kuondoka Kwa Hiari.

Posted on: June 5th, 2020


MKUU wa mkoa Rukwa Joachimu Wangabo amewataka Madiwani waliokaa muda mrefu katika nafasi hiyo kufikiria zaidi kustaafu nafasi hizo badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu kwenye mchakato wa uchaguzi na kuwa hiyo itawajengea heshima kubwa.

Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao cha baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya Nkasi kilicholenga kujadili hoja za ukaguzi ambapo amedai kuwa kimesalia kikao kimoja cha baraza hilo kuvunjwa kwa ajili ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu na kuwa sasa ni wakati wa kila mmoja kujitafakari nini amefanya katika eneo lake kabla ya kufikiri kugombea zaidi nafasi hiyo.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu ni ving’ang’anizi wa vyeo wakati nafasi hizo wanashindwa kuzitendea kazi na kuwa ufike wakati sasa kwao kujitafakari upya badala ya kuja kupata mshituko wa Moyo pale wanapoangushwa na wapinzani wao kwenye uchaguzi

“Mkae mkijua kuwa wapo watu huko nje wanahitaji kuingia ndani na nyie hamtaki kutoka hivyo kilichobaki sasa ni kujitafakari kwa kina kama mmetekeleza ipasavyo matakwa ya Wananchi kama ambavyo ilani ya CCM inavyosema na wale mliokaa muda mrefu kwenye udiwani ondokeni kwa hiari mpishe na wengine wenye mawazo mapya”. alisema

Lakini pia alitoa siku saba kwa mkurugenzi mtendaji kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua kali wale wote waliohusika kuisababishia halmashauri madeni kwenye makusanyo ya ndani (Defulters) na kuisababishia halmashauri deni la Mil.53.

Mwenyekiti wa halmashauri Zeno Mwanakulya kwa upande wake alisema kuwa ushauri wa mkuu wa mkoa ni vizuri ukazingatiwa na kuwa yeye mwenyewe binafsi anastaafu udiwani na hatagombea tena udiwani na kuwataka wenzie nao waliohudumu kwenye udiwani kwa mrefu waondoke na waingie wengine wenye nguvu mpya.

Alisema kuwa hapendi kuona madiwani wenzie aliofanya kazi nao wakiadhirika kwenye uchaguzi na kuwa ukiona kabisa huna nafasi ya kushinda tena kwenye uchaguzi ujao ni vizuri ukaondoka kwa heshima na jamii itakutambua na itaendelea kukutumia katika shughuli nyingine za kimaendeleo

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.