Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) Mkoani Rukwa wameanza uchimbaji wa visima vya maji kuanzia mita 60 katika vijiji vitano vya wilaya ya Kalambo ikiwemo kijiji cha Ilimba, Kanyezi,Lolesha ,Kasusu na Chalatila vitakavyo hudumia zaidi ya wakazi elfu kumi na moja (11000) wa wilaya hiyo.
Kaimu Meneja wa (RUWASA) wilayani humo Francis Mapunda amesema miradi hiyo inaenda kuondoa changamoto ya maji kwenye maeneo hayo na kuwataka wananchi kujenga mazoea ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji na miundombinu ya miradi ya maji ili kuifanya miradi hiyo kudumu kwa muda mrefu na kuleta tija katika jamii.
‘’Katika mwaka wa fedha 2022/22023 tuna mpango wa kuchimba visima vitano kwa awamu ya kwanza na mitambo kwa sasa ipo katika kijiji cha Ilimba ambako uchimbaji wa visima unaendelea na unatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 2500 wa kijiji hicho.
Kaimu meneja wa uchimbaji visima mkoani Humo Meshak Nyenza amesema, kwa awamu ya pili wanatarajia kuongeza vijiji 17 na kwamba kwa sasa wanachimba visima vyenye urefu wa mita 60 katika kijiji cha Ilimba.
Hata hivyo machi 2023 mkoa wa Rukwa ulipokea mtambo mmoja wa uchimbaji visima wenye uwezo wa kuchimba visima vyenye urefu wa zaidi ya mita 200 na kwa awamu ya kwanza visima 8 vitachimbwa katika wilaya ya kalambo na Nkasi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.