• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Safari Ya Maisha Ya Rais Mstaafu Wa Tanzania

Posted on: July 24th, 2020


Mwezi Novemba mwaka jana Mzee Benjamin Mkapa alitoa kitabu juu ya maisha yake, na katika aya ya mwisho ya dibajia aliandika kuwa anatumai kuwa kitabu hicho kitatoa mchango katika historia ya Tanzania na kuwatia moyo na kuwapa maarifa viongozi wa kesho wa Bara la Afrika.

Miezi minane toka atoe kitabu hicho, Mzee Mkapa ameaga dunia jijini Dar es Salaam na kuacha kitabu hicho kama kumbukumbu yake itakoyoishi milele.

Historia ya maisha yake, toka alipozaliwa mwaka 1938 na kukua katika familia ya kimasikini katika kijiji cha Lupaso, mkoa wa Mtwara mpaka kuwa rais ni simulizi ya kutia moyo.

Mkapa naeleza namna ambavyo ilimlazimu kutembea kwa umbali mrefu, miguu peku chini, kutafuta elimu katika shule za Wamishenari.

Baada ya kumaliza darasa la 10, sawa na kidato cha pili kwa mfumo wa sasa, Mkapa alitaka kuwa askari. Alipoulizwa na mwalimu wake wa kizungu kuhusu kuendelea na elimu mpaka darasa la 12 na kisha Chuo Kikuu, Mkapa anakiri kwenye kitabu chake kuwa hakujua kama kulikuwa na muendelezo huo wa masomo.

Baada ya kufaulu vizuri darasa la 12, Mkapa alienda Chuo Kikuu cha Uganda ambapo mwaka 1962 alihitimu Shahada ya Kingereza. Baada ya hapo alienda Marekani na kusomea diplomasia.

Alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania akianza ajira kama afisa wa wizara ya mambo ya nje na baadae kuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya chama na serikali pamoja na kuwa mwandishi wa rais Nyerere.

Mkapa pia alihudumu katika nafasi ya Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Canada na Marekani. Pia alikuwa waziri wa Mambo ya Nje katika vipindi viwili tofauti katika utawala wa Nyerere na baadaye rais wa pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.

Mkapa aliingia madarakani mwaka 1995 baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, baada ya kuhudumu serikalini kwa miongo mitatu.

Mwaka 1995 Mkapa alijitosa kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pasi kupigiwa upatu na watu wengi.

Katika kitabu chake, Mkapa anaeleza kuwa alimfuata aliyekuwa rais mstaafu wa Tanzania na Baba wa Taifa Hilo, Mwalimu Julius Nyerere kumfahamisha juu ya azma yake ya kugombea urais na sababu zake pia.

Mkapa anaandika kuwa baada ya kumsikiliza kwa makini Mwalimu alimjibu kuwa: "…Nitakuwa muwazi kwako. Sikutegemea kuwa ungetaka kuwania urais, wazo kama hilo halikuniingia kabisa."

Lakini si hivyo tu, Nyerere alimweleza Mkapa kuwa kuna mtu mwengine ambaye ailikuwa akimfikiria kuwa angekuwa rais bora, lakini alikuwa akisita kuingia kwenye mchuano huo. "Ben, kitu pekee ninachokuahidi ni kuwa sitakuzibia njia, sitakupinga."

Mkapa alishinda uchaguzi ndani ya chama akipata ushindani mkali kutoka kwa Jakaya Kikwete (ambaye alikuja kumrithi madaraka ya urais mwaka 2005).

Alishinda uchaguzi mkuu kwa asilimia 61.8 ya kura, huku kinara wa upinzani katika uchaguzi huo akiwa Augustino Mrema akipata 27 Augustino Mrema akipata asilimia 27.7 ya kura..

Hata baada ya kuondoka madarakani mwaka 2005, Mzee Mkapa aliendelea na utumishi kwa nchi yake na jamii ya Kimataifa.

Uchaguzi wa urais nchini Kenya wa mwaka 2007 ulifuatiwa na ghasia kubwa mabzo zilitishia ustawi wa Taifa hilo. Mzee Mkapa alikuwa ni mmoja wa viongozi kutoka barani Afrika ambao waliwahi na kuchukua jitihada za kuwaweka pamoja mahasimu wa kisiasa Raila Odinga na Mwai kibaki katika meza ya mazungumzo.

Japo kazi hiyo ya usuluhishi ilikuwa ngumu lakini mwishowe ikazaa makubaliano na kuundwa kwa serikali ya mseto na hatimaye kurejesha utulivu nchini humo.

Mkapa pia amehudumu kama msuluhishi katika mgogoro wa kisiasa Burundi pamoja na harakati za uhuru za Sudani Kusini.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.