Sehemu ya msitu wa hifadhi ya maporomoko ya mto Kalambo mkoani Rukwa imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa ikidaiwa kuwa moto huo ulitokea katika kijiji cha kipwa kilichopo mpakani mwa nchi yaTanzania na Zambia na hivyo kuambaa hadi kwenye kingo za hifadhi iliyoko upande waTanzania.
Akithibitisha tukio hilo, Afisa mistu Msaidizi katika eneo hilo Moses Kazimoto, amesema moto huo umeharibu miundo mbinu ikiwemo bomba za maji pamoja na uoto wa asili ambao kiikolojia ni kivutio kikubwa, na kuwataka wananchi kuilinda hifadhi hiyo kwa bidii kwani ni sehemu ya urithi wa nchi.
Mkuu wa Wilaya ya KalamboJulieth Binyura amesema atawachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakao bainika kuhusika na tukio hilo na kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa kuzima moto kila unapozuka pamoja na kutoa taarifa kwenye uongozi ili hatua za haraka zichukuliwe.
‘’Moto umeharibu kabisa uoto wa asili kama tunavyo ona, nachukua fursa hii kuwa asa wananchi kufanya kazi zao kwa makini na kuepuka kuchoma moto hasa wakati huu wa maandalizi ya mashamba.Tujue kuwa kwenye hifadhi hii kuna wanyama wengi wakiwemo Tembo ambao hupata shida kubwa na wakati mwingine kuangamia kwa majanga kama haya ya moto.
‘’Upande wetu sisi kama Serikali Wilayani Kalambo, tunapinga vikali tabia hii na tunasema wazi kuwa hatuta sita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kufanya hujuma hii.’’
Maporomoko ya mto Kalambo ni ya pili Afrika kwa urefu kutoka maji yanapoanzia kumwagika hadi yanapodondokea kwa mita 235 na upana wa mita 3.6 hadi mita18.Hivyo yakitunzwa vizuri watalii kutoka sehemu mbalimbali watafika na hivyo kukuza uchumi hasa wakati huu ambapoTanzania inajiandaa kuingia kwenye uchumi wa kati .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.