• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Serikali Kuanza Ujenzi Wa Miradi Mitatu Ya bandari Katika Wilaya Kalambo na Nkasi .

Posted on: August 5th, 2019


Mamlaka ya Bandari hapa nchini imeanza utekelezaji wa miradi mitatu ya bandari katika Mkoa wa Rukwa inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 .7 katika ya wilaya ya kalambo na Nkasi.

Akiongea mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo katika  eneo la kipili  wilayani  Nkasi, mkuu  wa  mkoa huo Joachim Wangabo  amesema   kuna  kila  sababu  ya wizara ya  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na wananchi wanaoishi katika mwambao wa Ziwa Tanzganyika.

Mh. Wangabo amesema kuwa wananchi hao wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutumia vyombo kama mitumbwi na boti ambavyo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na meli kubwa ya MV Liemba ambayo usalama wake ni wa uhakika.

“Nitoe wito kwa wizara husika hii meli ya MV Liemba nimeambiwa hapa kwamba ikipita kwenda Zambia inaitwa ‘Our Baby’ mtoto wetu, sasa huyu mtoto wetu anaulizwa yuko wapi, Zambia wanauliza, sasa Wizara husika twende haraka isimamie hili jambo, MV Liemba itengenezwe, watu maisha yao yapo kwenye hatari kubwa ndani ya hili ziwa Tanganyika”

Naye Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mh Ali Kessy alieleza kuwa meli hiyo ya MV Liemba ilitakiwa kukamilishwa ukarabati wake tangu mwaka wa fedha 2017/2018 lakini fedha za ukarabati hazikutengwa na kudai kuwa Waziri wa Fedha Mh. Filipo Mpango amemuhakikishia kuwa fedha za ukarabati wa meli hiyo zimetengwa katika bajeti yam waka 2018/2019.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Pasivo Ntetema amesema kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa gati, jengo la kupumzikia abiria, jengo la mgahawa, ofisi, ghala la kuhifadhia mizigo, nyumba za wafanyakazi na uzio na kuongeza kuwa kwa Bandari ya Kabwe peke yake wastani wa usafirishaji kwa mwezi ni tani 1500 hadi 2000 na mwaka wa fedha 2018/2019 zimesafirishwa tani 20,000

“Pamoja na changamoto za miundombinu lakini utaona kuna ‘access’ nzuri ya watu kupita hapa kwahiyo kukishaboreshwa bandari hii ikakamilika lakini pia miundombinu ya barabara ya kuingia hapa ikakamilika ni Imani yetu watu wa bandari ya kwamba kupitia uongozi wako, kupitia mheshimiwa mbunge na mamlaka zote zinazotawala mkoa wa Rukwa pamoja na serikali kuu, tutaangalia sasa uwezekano wa kuboresha barabara hii kwa kiwango cha lami ili shehena kubwa iweze kupita hapa

Mamlaka ya Bandari inatekeleza miradi mitatu katika Mkoa wa Rukwa ambayo ni Mradi wa uboreshwaji wa bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo, Ujenzi wa barabara katika Bandari ya Kipili na Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Gati Bandari ya Kabwe zilizopo katika Wilaya ya Nkasi ambapo miradi yote itagharimu shilingi bilioni 12.7

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.