Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Rukwa imeendelea na zoezi la kufanya uhakiki wa maeneo ya wazi na maeneo ya umma yaliyoorodheshwa kwa mujibu wa ramani za mipango miji za halmashauri za mkoa huo ili kubaini endapo kuna uvamizi umefanyika katika maeneo hayo.
Akiongea kuhusiana na zoezi hilo Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kupata orodha kamili ya meneo ya wazi ili yaweze kutambulika rasmi huku akiwaonya wananchi waliovamia katika maeneo hayo.
“Kwa maeneo ambayo yatakuwa yamevamiwa, kutakuwa hakuna namna ya kufanya isipokuwa wavamizi wataondolewa ili kupisha maeneo ya wazi kwasababu yanatakiwa yalindwe kwa nguvu zote, na maeneo ambayo yapo salama mpaka sasa hivi tutahakikisha mipaka yake inawekwa bayan ana wananchi watatakiwa waiheshimu,” Alisema.
Aidha aliongeza kuwa baada ya kupata orodha ya kamili ya maeneo hayo atakabidhiwa Mkurugenzi ili aweze kuyaandalia hati kwaajili ya ulinzi wa maeneo hayo kwa siku za usoni.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.