Serikali mkoani Rukwa imesema ina ziada ya chakula 470,793.6 baada ya msimu wa mavuno wa mwaka 2019, 2020 kufanikiwa kuvuna tani 884,368.8 ikiwa ni sawa na asilimia 69 ya mavuno yote na kusisitiza wananchi kuendelea kulima mazao kwa kushirikina na wataalamu.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo jana alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akiwatoa hofu wananchi wa mkoa huo kuhusiana na kuwepo kwa tishio la upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Alisema kuwa mkoa wa Rukwa unatarajia kutumia tani 413,575 kwa mwaka 2019,2020 na kubakiwa na ziada hiyo ya chakula hivyo mkoa huo unachakula cha kutosha na hakuna hofu yoyote katika hilo.
Wangabo alisema kuwa hata hivyo uzalishaji umeshuka kwani mkoa ulitarajia kupata chakula tani 1,677,474.8 lakini ulipata tani 1,164,242.42 hata hivyo pamoja na kutofikia lengo la uzalishaji kwa asilimia mia moja lakini bado kuna ziada hiyo ya chakula.
Alisema kuwa tayari serikali kupitia wakala wa hifadhi ya chakula(NFRA) imetoa fedha kwaajili ya kununua tani 18,000 ya chakula ambapo mkoa wa Rukwa itanunua tani 13,000 na katika mkoa wa Katavi itanunua tani 5,000 kwaajili ya kuhifadhi.
‘’katika msimu wa ununuzi wa 2019/2020 wakala wa hifadhi ya chala na cha taifa kanda ya sumbwanga umepangiwa kununua mahindi kiasi cha tani 18,000 kati ya hizo tani 13,000 ni kwamkoa wa Rukwa na ununuzi utafanyika Namanyere kwa wilaya ya Nkasi,Mwimbi na Matai kwa wilaya ya Kalambo ,mazwi ,mtowisa na laela kwa wilaya ya Sumbawanga’’alisema wangabo.
Naye Richard Luah afisa ugavi wa NFRA mkoa wa Rukwa alisema kuwa mwaka huu serikali itanunua kilo moja shilingi 500 ambapo gunia la kilogramu 100 litanunulia kwa shilingi 50,000 bei ambayo itakuwa nzuri tofauti na walanguzi ambao wamekuwa wakiwalalia wakulima na kununua gunia hilo hadi shilingi 18,000.
Aliwaomba wakulima kuhakikisha wanazingatia ubora wa mazao hayo kwa kuwasafisha na kuyakausha vizuri sambamba na kuacha tabia ya kuchanganya na uchafu mwingine ili yawe mazito kwani wanaweza wasifanikiwe kuyauza mazao hayo hususani mahindi kutokana na kushindwa kukidhi ubora.
Aliwasihi wakulima kuhakikisha kuwa wanauza mazao yao mapema ili wapate fedha kwaajili ya kuanza kununua pembejeo za kilimo kwaajili ya msimu ujao kwani wakiiacha fursa hiyo watauza mazao yao kwa bei mbaya na matokeo yake watashashindwa kufanya vizuri katika msimu ujao wa kilimo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.