Wananchi washio katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujenga mazoea ya kupanda miti kuzunguka maeneo yao ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba imara ambazo zitakuwa na uwezo wa kuhimili vishindo vya upepo mkali ambao umekuwa ukijitokeza na kuezua nyumba zao.
Wilaya ya Kalambo ina vijiji 9 vinavyo patikana katika mwambao wa ziwa Tanganyika ambapo baadhi ya vijiji hivyo vimekuwa vikikumbwa na maafa ya mafuliko ambayo yamekuwa yakitokana na mabadiliko ya tabia ya nchi hususani kujaa maji katika ziwa Tanganyika.
Hata hivyo Februari 6/2022 kulijitokeza maafa katika vijiji vya Kisala na Samazi katika mwambao wa ziwa hilo ,ambapo nyumba zipatazo 27 ziliezuliwa na upepo mkali ambao ulijitokeza majira ya saa kumi na moja alfajiri na kusababisha familia 10 kukosa makazi huku kati ya hizo nyumba 10 zikiezuliwa katika kijiji cha Kisala na nyumba 17 zikiezuliwa katika kijiji cha Samazi.
Wataalam wa Halmashauri ya Kalambo walifika eneo la tukio na kuangalia madhara yaliyotokana na maafa hayo, ikiwa ni pamoja na kuwafariji wananchi waliokuwa wameathirika na maafa hayo na kufanya tahimini ya kuezuliwa kwa nyumba hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ilotolewa na Idara ya Maendeleo ya jamii wilayani humo ilibainisha hasara iliojitokeza kutokana na maafa hayo ikiwemo uharibifu wa kiwanda cha samaki Samazi kuezuliwa na kupata hasara ya Tsh 15,000,000/=, huku nyumba zilizo athirika zikiwa na hasara ya Tsh 8,100,000/= na kufanya jumla ya Tsh 23,100,000/=.
Awali akiongea mara baada ya kuwatembelea waathirika wa maafa hayo kwenye vijiji hivyo, katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe, aliwataka wananchi kujenga mazoea ya kupanda miti ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba imara kwa kutumia sementi kama njia ya kuepukana na kadhia hiyo kutojirudia.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.