Wakulima wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelalamikia kucheleweshwa kwa pembejeo pamoja na bei elekezi katika msimu huu wa kilimo hali inayotia hofu kutopata mavuno kutokana na wakulima wengi kulima bila kutumia pembejeo.
Mmoja wa wakulima hao Samu Mwasomola, alisema kuwa kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo kitendo kinachopelekea wakulima kutumia mbegu zisizo faa na zisizo na ubora.
Naye Edwini Mwasabwite, alisema kuwa wanaiomba serikali kuwa na mazoea ya kuwahisha pembejeo za kilimo kabla ya msimu kuanza kwa lengo la kuwawezesha wakulima kupata mazao mengi na kuondokana na adha ya kutumia pembejeo zisizo na ubora.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kalambo Nikoraus Mrango, alisema kuwa serikali imesambaza pembejeo za kilimo katika maduka yote yanayouza pembejeo sambamba na kutoa bei elekezi.
Alisema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kukagua kama pembejeo hizo zinawafikia wakulima na kuwataka wakulima kutoa taarifa endapo kuna changamoto zinazowakabili katika maeneo yao husika.
‘’tutachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria endapo kuna wauzaji wa pembejeo watakao bainika kukiuka taratibu wakati wa kuwauzia pembejeo wakulima’’alisema Mrango.
Awali akiongea kupitia madhimisho ya msimu wa kilimo mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliwataka watendaji wa Halmashauri hiyo kusimamia na kuhakikisha wauzaji wa pembejeo wanauza pembejeo za kilimo kwa bei elekezi.
Pia alisema wilaya inaendelea kusisiza wakulima kulima kibiashara mazao mbalimbali ikiwemo Alizeti na kahawa ili kuongeza wigo wa mazao yanalimwa na kupunguza utegemezi kwenye zao la mahindi ambalo wakati mwingie bei yake imekuwa haitabiliki.
Hivi karibuni mkoa wa Rukwa ulizindua msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2019/20 na unakusudia kulima hekta 603,637.13 za mazao mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na uhakika wa chakula.
Mwisho
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.