- Wizara ya mifugo na uvuvi hapa nchini imesema inategemea kuanza kuboresha miondombinu ya soko kuu la samaki Kasanga lilipo wilayani kalambo mwambao wa ziwaTanganyika mkoani Rukwa ambalo litahudumia zaidi ya wananchi elfu kumi na nane wa kata za kasanga naSamazi kwa lengo la kusaidia kuboresha uchumi wa wananchi pamoja na kuongeza thamani ya samaki.
Mradi wa ujezi wa soko la Samaki kasanga ulianza kutekelezwa mwaka mwaka 2009 na kukamilika mwaka 2011 na kugharimu kiasi cha zaidi ya shilingi millioni 876 na huku lengo kuu la mradi huo ikiwa ni kupata wanunuzi wa uhakika wa samaki wa ndani na nje ya nchi pamoja na kusaidia kuongeza pato la halmashauri na serikali kuu.
Akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mkurugezi mtendaji wa halmshauri ya kalambo Msongela Palela alisema ukosefu wa miondombinu ya barabara pamoja na umeme umekuwa kikwazo kikubwa kutofanyika kwa biashara maeneo hayo .
‘’kumekuwa na changamoto ya walengwa kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uvuvi endelevu unaozingatia tija na mazingira ya ziwa Tanganyika na mwambao wake kwa ujumla, pia uhaba wa zana na vifaa vya vya uvuvi hali inayopelekea soko kutokamika kwa kiwangokinachostahili’’alisema palela
Alisema kukamilka kwa miundombinu iliosalia kutawezesha kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi kwa kiwango kikubwa kinachotakiwa kwa kufuata sheria.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe amesema tayari wamefanya mawsilino na shirika la Tanesko na wamekubali kupeleka umeme kwa gharama zao kwenye maeno hayo.
‘’julay saba 2019 naibu waziri wa tamisemi alifika katika maeneo hayo lakini baada ya kuondoka tu shirika la tanesiko nalo lilifika na vifaa vyote tayari kwa kuweka umeme maeneo haya, hali hii inasaidia kujenga imani kwa wananchi kuona serikali inawatimizia mahitaji yao kwa muda muafaka.’’alisema sichalwe.
Awali akikagua mradi wa soko hilo katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi DKT Rashid Tamatama amesema lengo la kujengwa kwa masoko hayo ni kuongeza thamani ya samaki wanavuliwa kwenye ziwa Tanganyika.
Alisema kukamilika kwa miundombinu iliosalia kwenye maeneo hayo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza thaamani ya samaki ambao wamekuwa wakivuliwa kwenye ziwa hilo.
Licha ya hilo katibu huyo ametembelea na kukagua uendeshwa wa kiwanda cha samaki muzi kichopo mwambao wa ziwa hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.