Serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira RUWASA imeanza ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la maji wenye thamani ya shilingi billion 1,770,686,091.83 utakao hudumia zaidi ya vijiji 5 na watu elfu kumi na mbili (12000) katika kata ya mbuluma wilayani kalambo mkoani Rukwa.
Akiongea Wakati Wa Ukaguzi Wa Maradi Wa Bwawa Hilo Kaimu Meneja Wa Ruwasa Wilayani Humo Mhandisi Marwa Webiro Amesema Mradi Huo Utahusisha Ujenzi Wa Tuta La Bwawa Na Ujenzi Wa Utoro Wa Maji Mita 368 Na Kusema Mpaka Sasa Kazi Zilizo Fanyika Ni Pamoja Na Usafishaji Wa Eneo Sambamba Na Upimaji Wa Alama Za Tuta Lenye Urefu Wa Mita 368 Na Pimaji Wa Mita Za Mianguko Ya Maji.
Kamati Ya Siasa Ya Chama Cha Mapinduzi Ccm Wilayani Humo Imefanya Ukaguzi Wa Miradi Huo,Ambapo Mkuu Wa Wilaya Ya Kalambo Lazaro Komba , Amesema Mradi Huo Utahudumia Vijiji 5 Vyenye Idadi Ya Watu 12000 Kwa Gharama Ya Shilingi Billion Moja 1,770,686,091.83.
Awali Akiongea Wakati Wa Ukaguzi Wa Mradi Huo Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Wilayani Humo Vitus Nandi, Licha Ya Kuipongeza Serikali Kuwa Kutoa Fedha Hizo Amewataka Maafisa Wa Idara Ya Maji Kuharakisha Mradi Huo Ili Uweze Kukamilika Kwa Wakati Na Kuwawesha Wananchi Kuendelea Kunufaika Na Huduma Ya Maji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.