Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema Serikali inakusudia kuanza uboreshaji wa mpaka wa kasesya unaounganisha kati ya nchi ya Tanzania na Zambia ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Matai Kasesya kwa kiwango cha Lami.
Ameyasema hayo baada ya kutembelea Kituo cha forodha cha Kasesya Wilayani Kalambo Mkoani humo na kusema serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 inakusudia kuanza ujenzi wa majengo mapya ya Taasisi za umma ikiwemo kituo cha polisi, uhamiaji , majengo ya ukusaji mapato (TRA) Pamoja na nyumba za watumishi.
Licha ya hilo Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wananchi Wilayani humo kukamilishwa kwa Barabara ya Matai Kasesya ikiwa ni Pamoja na kuboreshwa kwa bandari ya Kabwe kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa mizigo Kwenda katika nchi jirani ikiwemo Kongo, Zambia na Burundi.
Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2024-2025 kituo cha forodha Kasesya Wilayani Kalambo kilifanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya kiasi cha shilingi billion 25.7 sawa na asilimia 172 kati ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi billion 14.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.