Serikali imeanzisha kampeni ya utoaji wa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo na utambuzi kwa kuweka hereni za kielekitronic kwenye mifugo hatua itakayo Saidia kutomkomeza magonjwa ya homa za mapafu.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Dkt Lazaro Komba kupitia uzinduzi wa kampeni hiyo iliofanyika katika kijiji cha Katuka kata ya Msanzi wilayani humo amesema licha ya zoezi hilo linahusisha uchanjaji wa kuku na mifugo jamii ya ng’ombe dhidhi ya ugonjwa wa homa ya mapafu.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kuzingatia chanjo kwenye mifugo yao ikiwa ni Pamoja na kufuga kwa tija ikiwemo kuzalisha mbegu bora ambazo zitawawesha kuinuka kiuchumi.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa mifugo wilayani humo Dkt. Enos Luvinga amebainisha kuwa lengo la serikali ni kupunguza gharama za matibabu, vifo vya mifugo ikiwa ni Pamoja na kuongeza upatikanaji wa mazao yatokanayo na mifugo ikiwemo nyama na maziwa ambayo husaidia kuboresha afya ya mwili.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.