SERIKALI nchini imefunga machio ya nyama katika manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kutokana na kutokidhi vigezo ya kuwa kalo ya kuchinjia mifugo.
Akifunga machinjio hayo Kaimu msajili wa bodi ya nyama nchini,Imani Sichwale,amesema kuwa kalo hiyo ya mifugo haina vigezo vya kuhifadhia nyama na kusema kuanzia sasa inafungwa rasmi.
‘’kalo hii haina vigezo na kibaya zaidi imejengwa katikati ya mji hivyo kuanzia leo imefungwa na mkurugezi atawatafutia njia mbadala.’’alisema
Alisema kwa kawaida nyama haitakiwi kugusa chini wala kuchinja mifugo ikiwa chini kwani kwa kufanya hivyo kunafanya walaji wa nyama kula nyama chafu.
Alisema kuwa Manispaa kutumia kalo kama machinjio ni kosa na kusema kuwa suala hilo atalipeleka kwa mkurugezi ili awatafutie wachinjaji sehemu mbadala ya kuchinjia mifugo yao.
Kwa upande wa wakazi wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamelalamikia kufungwa ghafla kwa muda usiojulikana machinjio ya mifugo ya Manispaa hiyo kitendo kitakacho sababisha kukosekana kwa kitoweo cha nyama katika mji huo.
Wamesema kuwa machinjio hayo ndiyo yanayotegemewa na wakazi wa Manispaa hiyo kwa na kufungwa bila kuwa na eneo mbadala kunaweza kusababisha kukosekana kabisa kwa kitoweo cha nyama, hivyo kuiomba serikali kuteua eneo mbadala ili kuwawezesha wakazi hao kuendelea kupata kitoweo kama ilivyo kuwa hapo awali.
Alex mwita ni mmoja wa mkazi wa mji wa Sumbawanga, alisema kuwa serikali haina budi kuweka utaratibu maalumu utakao wawezeaha wao kupata kitoweo hicho kwani walikuwa wamezoea kwenda kununua nyama kwenya machinjio hayo lakini kufungwa kwake kutafanya kukosa mboga ya kutumia majumbani.
"Machinjio imefungwa ghafla sana,nafikiri kwamaoni yangu serikali ingetafuta njia mbadala ya kutunusuru na suala hili kwani hatuelewi tutapata wapi tena kitoweo cha nyama kutokana na kuwa awali tulikuwa tukitegemea hapa’’ al
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.