Naibu waziri wa wizara ya uchukuzi Mhe.David Kihenzile amesema serikali imeidhinisha fedha kiasi cha shilingi Billion 600 kwa ajili ya ujenzi wa meli yenye ukubwa wa tani 3500 itakayo kuwa ikifanya safari zake katika ziwa Tanganyika kupitia bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua miundombinu ya bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kusema licha ya hilo serikali inakusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza meli kubwa ambayo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi meli mbili zenye ukubwa wa tani 500 kwa wakati mmoja.
Pamoja na hayo amesema serikali imeanza ukarabati wa meli tatu za mizigo na abiria ikiwemo meli ya MV.Liemba,MV.muongozo na MT.Sangala ambazo zikikamilika zitarahisisha swala la usafiri na usafirishaji wa mizigo katika ziwa Tanganyika.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.