Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewataka wananchi mkoani humo kuwa sehemu ya kutunza na kulinda miundombinu ya barabara na madaraja zinazo jengwa na serikali ili kuifanya miradi hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa daraja linalounganisha kijiji cha Nondo na Kasitu wilayani Kalambo lenye urefu wa mita 80 na kujengwa kwa gharama ya shilingi 4,763,3311,591.50 na kusisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo vya dora dhidi ya watu wanao haribu na kuiba vyuma kwenye madaraja.
Meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Daudi Kaigi ,amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia mia na mkandarasi amelipwa jumla ya fedha shilingi 3,558,440,044.67 ikiwa ni malipo ya awamu mbili.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Shafi Mpenda amesema uwepo wa daraja hilo utarahisisha shughuli za ukusanyaji mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kuwa kichocheo cha watalii kutokana na daraja hilo kuunganisha na daraja la mto huo.
Licha ya hilo mkuu wa mkoa ametembelea na kukagua ujenzi wa shule ya msingi Matai Asilia katika kata ya Matai pamoja na ujenzi wa mradi wa barabara ya Matai Kisungamile inayojengwa kwa kiwango cha Lami kwa gharama ya Tsh,829,765,068,63.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.