Serikali mkoani Rukwa imekamilisha ujenzi shule mpya 12 za msingi na sekondari ambazo zimejengwa kwa thamani ya shilingi billion 6.064 na kuwawesha wanafunzi wa darasa la kwanza 30.922 sawa na asilimia 60.2 Kuanza masomo ya elimu ya msingi
Mapema akiongea ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema kwa upande wa Darasa la awali mkoa ulilenga kuandikisha Wanafunzi 57,006 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 27,885 na jinsia ya kikeake wakiwa 29,121) ambapo hadi kufikia tarehe 04 Januari, 2024 Wanafunzi 24,033 wa Darasa la awali sawa na asilimia 42.1 walikuwa wameandikishwa kuanza darasa la awali.
‘’ Kwa upande wa Darasa la kwanza Mkoa ulilenga kuandikisha Wanafunzi 51,347 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 25,254 na jinsia ya kike wakiwa 26,093) ambapo Mpaka tarehe 04 Januari, 2024 Jumla ya Wanafunzi 30,922 walikuwa wameandikishwa kujiunga na darasa la kwanza sawa na asilimia 60.2’’. alisema Makongoro.
Aidha amesema Kwa upande wa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu Jumla ya Wanafunzi wa Darasa la awali 167 kati yao jiansia ya kiume wakiwa 69 na wakike 98) wameandikishwa na kwa upande wa Darasa la kwanza kwa Wanafunzi wenye Mahitaji maalum jumla ya Wanafunzi 91, wameandikishwa.
Hata hivyo Jumla ya Wanafunzi 31,182 waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la Saba mwaka 2023, kati ya hao Wavulana walikuwa 13,946 na Wasichana 17,236 sawa na asilimia 97.2 baada ya matokeo ya Mtihani Jumla ya wanafunzi/watahiniwa 24,415 wakiwemo wavulana 11,270 na wasichana 13,145 walifaulu sawa na asilimia 78.30 na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro Komba kupitia kaguzi za wanafunzi mashueni ,alisema wilaya ya Kalambo imefanikiwa kukamilisha vyumba 39 vya madarasa vyenye thamani ya shilingi billion 1.3 sambasamba na kujenga nyumba 2 za walimu zenye thamani ya shilingi milioni 200 na bweni la shule ya msingi Msanzi A litakalo hudumia wanafunzi 600 wenye mahitaji maalumu.
Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shule na kuendelea na masomo yao na kusema serikali haita sita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wazazi na walezi ambao watashindwa kuwapeleka watoto shule.
Awali akiwa katika shule ya msingi Kirando wilayani Nkasi Mkoani Rukwa Mkuu wa wilaya ya Hiyo Piter Lijualikali , alisema wanafunzi wote waliokuwa wameandikishwa wameripoti shule na kundelea na masomo na kuipongeza serikali kwa kukamilisha vyumba vya madarasa ambavyo vimewesha wanafunzi wengi zaidi kuanza masomo kwa mwaka 2024.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Sumbawanga akiwemo Braun Mtawa ambao licha ya kuipongeza serikli kwa kuwekeza fedha nyingingi kwenye ujenzi vyumba vya madarasa ,wameishauri serIkali kuona uwezekano wa kuongeza idadi ya walimu wa shule za msingi ili kuendana na ongezeko la madarasa na wanafunzi wanao ripoti shule.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.