SERIKALI imeonya vikali dhidi ya mtu yeyote, hasa watumishi wa umma na wachanjaji, watakaojaribu kuwatoza wafugaji fedha kwa ajili ya huduma za chanjo na utambuzi wa mifugo, ambazo kwa mujibu wa Serikali, zinatolewa bure kwa asilimia 100.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, kupitia zoezi la utoaji chanjo katika Ranchi ya Taifa ya Kalambo (NARCO) wilayani Nkasi mkoani Rukwa ameeleza kuwa shughuli zote za kuchanja na kutambua mifugo zinagharamiwa kikamilifu (kwa asilimia 100) na Serikali.
Aidha amesema Zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa, ambapo hadi kufikia tarehe 9-7-2025 ng’ombe wapatao 1,500 wamechanjwa ikiwa ni Pamoja na kutoa chanjo kwa wafugaji juu ya umuhimu wa chanjo na matumizi ya teknolojia ya kidijitali kwenye utambuzi wa mifugo ili kulinda usalama wake na kusaidia Serikali kuwa na takwimu sahihi kwa mipango ya kisera, kisheria na kiuwezeshaji.
Pamoja na mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa zoezi hilo kuzingatia maadili na kuacha tabia ya kutoza wafugaji pesa kwani ni kinyume cha sheria na miongozo ya Serikali kwa kuwa gharama zote zimelipwa na Serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.