SERIKALI mkoani Rukwa imesema imejipanga kufanya ukarabati wa madaraja yote yaliyoharibika yakiwemo ya vijiji vya kata ya Mbuluma Wilayani Kalambo na mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawanga na huku ikiwasisitiza wananchi kuto pita maeneo yenye maji mengi kwa lengo la kuondokana na matatizo yasiokuwa yalazima.
Hatua hiyo inakuja kufutia Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha mkoani humo na kusababisha adha kwa wananchi ikiwa ni pamoja na vifo vya watu wawili katika vijiji vya Kanyalakata na Chisenga Wilayani ya Kalambo, tukio lililo ambatana na kubomoka kwa nyumba saba katika kata ya Kasanga huku ikisababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya Kasisiwe katika Manispaa ya Sumbawanga na kupelekea mama mja mzito kujifungulia vichakani baada ya mto huo kujaa maji na kushindwa kupita akiwa njiani kuelekea hospitalini.
Kalambodc imezungumza na meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini TARULA mkoani humo Seth Mwakembe na kusema yafuatayo;
‘’Nikweli katika kipindi hiki cha masika Tanzania imekumbwa na mafuriko katika maeneo mbalimbali na sehemu kubwa imeathiri ni miundo mbinu ya madaraja. Lakini mpango wa serikali ni kuyakagua madaraja yote na kuangalia uharibifu kwa lengo la kuyakarabati ili yapitike .
‘’Kuna maeneo yameathirika kwa kiasi kikubwa kuliko hata madaraja ya Mbuluma na Kasisiwe hivyo niwatake wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati Serikali ikijiandaa kufanya ukarabati huo ikiwa ni pamoja na kuto pita sehemu zenye maji mengi au kusubiri maji yapungue ndipo wavuke.’’ Alisema Mwakyembe.
Akiongea kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, aliwataka wananchi kuwa makini katika kipindi hiki kwa kuacha maji yapite ndipo wavuke kwenye mito iliyojaa ili kuepukana na matatizo yasiyo kuwa yalazima.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.