Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameziagiza Halmashauri Mkoani humo kupanda miti milioni sita katika mwaka 2018. hayo ameyasema katika Sherehe za kilele cha upandaji miti katika Mkoa wa Rukwa zimefanyika katika shule ya sekondari Matai Wilaya ya Kalambo tarehe 19 Januari 2018, na kuhudhuriwa na viongozi na wataalam mbalimbali wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri pamoja na wananchi huku Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa ni Mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Katika sherehe hizo hotuba ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa zilijikita katika mambo mbalimbali yenye lengo la kulinda mazingira yetu. Mambo hayo ni kuwasihi wananchi na Taasisi mbalimbali Kupanda miti mingi kadri iwezekanavyo huku kiwango cha kitaifa kikiwa ni kupanda miti Milioni Moja na Nusu kila mwaka kwa kila Halmashauri. Katika upandaji miti Mkuu wa Mkoa amehimiza upandaji miti ya matunda na mbao kwa lengo la kulinda afya na kuongeza kipato kutokana na mazao ya miti hiyo.
Pia Wananchi wamehaswa kutochoma miti na misitu pindi wanapotekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo mbalimbali, mamlaka za Serikali kuwaondoa wananchi katika hifadhi mbalimbali, wataalamu wa Misitu kushauri juu ya miti inayofaa kupandwa katika mazingira mbalimbali, kufanya ufuatiliaji wakina katika maeneo ambayo miti imepandwa ili kuhakikisha miti inakua. Kutoa elimu katika shule juu ya utunzaji mazingira, Taasisi mbalimbali kusimamia misitu ya kupandwa pamoja na asili, Wakala wa misitu Nchini (TFS) kusimamia sheria kwa ukaribu ikiwa ni sambamba na kuotesha miti. Wananchi na Taasisi mbalimbali kuwaripoti waaribifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Aidha katika sherehe hizo wadau mbalimbali wa mazingira walipata nafasi ya kusema maneno machache juu ya namna wanavyohusika kwa namna moja au nyingine katika utunzaji wa Mazingira katika Mkoa wa Rukwa. Moja ya wadau wa Mazingira Mkoa wa Rukwa taasisi ya REYO ilihahidi kutoa mishe ya miti mbalimbali pamoja na miti ya matunda kwa Kijiji kimoja katika kila Wilaya ya Rukwa ikiwa ni lengo la kuiunga mkono Serikali katika utunzaji wa Mazingira.
Sherehe hizo zilihitimishwa kwa zoezi la kupanda Miti katika eneo ya shule ya sekondari Matai lenye ukubwa na heka mbili, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliongoza zoezi hilo na kuwasihi wananchi kuwa zoezi la upandaji miti ni endelevu hivyo lisikome katika sherehe hizo, eneo hilo limepewa jina la msitu wa Wangabo ikiwa lengo la kuwaenzi viongozi wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akipanda miti
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Daud Sichone akipanda miti
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mhandisi Simon C. Ngagani akipanda miti
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.