Shule ya msingi Kipanga iliyopo wilayani Kalambo Mkoani Rukwa imekabidhiwa ngao ya ushindi baada ya kushika nafasi ya kwanza ya ufaulishaji mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2023 ikifuatiwa na shule ya sekondari Zengwa ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika ufaulishaji mitihani ya kidato cha pili kwa mwaka 2023 na kukabidhiwa ngao ya ushindi.
Licha ya hilo shule ya Sekondari Kasanga imekabidhiwa cheti cha pongezi baada ya kufaulisha vizuri mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2023 baada ya kushika nafasi ya tatu kwa ngazi ya mkoa na kuifanya wilaya ya Kalambo kuwa miongoni mwa wilaya za mkoa wa Rukwa zilizo fanya vizuri kwa ngazi ya mkoa na taifa.
Hata hivyo shule hizo zilikabidhiwa ngao na vyeti na mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere kupitia kikao cha wadau wa elimu kilicho fanyika katika manispaa ya sumbawanga, ambapo aliwasisitiza walimu kufanya kazi kwa weredi ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.