Baadhi ya wananchi katika mji wa Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelazimika kuyahama makazi yao nyakati za usiku baada ya maji kujaa hadi kufikia usawa madirisha kufuatia mvua kubwa ilionyesha usiku wa kuamkia Desember 29,2019.
Kwa mujibu wa afisa tarafa ya Kasanga Endrue Manyema Ngindo , amesema baadhi ya nyumba za kulala wageni pamoja na nyumba za wananchi ziliweza kujaa maji na kupelekea kuyahama makazi yao.
‘’baadhi ya nyumba za kulala wageni ikiwemo ya Atupenda ‘’A’’ inayomilikiwa na Rhoda Maseba ilikuwa ndani ya maji usawa wa madirisha na kusabisha wateja wake kuhama usiku huo’’alisema Ngindo.
Aidha aliongeza kwa kusema nyumba ya Dorcas Nakazwe moja ya ukuta wa nyumba yake ulibomoka na kupelekea wapangaji wake kukimbia usiku huo .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.