Tasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa (TAKUKURU) mkoani Rukwa inawashikilia watu wanne akiwemo tabibu msaidizi wa kituo cha afya Matai wilayani Kalambo,Eliudi Joshua kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kiasi cha sh (100,000/=) kwa mgonjwa na kisha kumfanyia upasuaji bandia.
kamanda wa takukuru mkoa wa Rukwa,Hamza Mwenda amebainisha kuwa tukio la kwanza limetokea wilaya ya Kalambo,ambapo tatibu msaidi wa kituo cha afya Matai alikamatwa na amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa na kumfanyia upasuaji bandia mgonjwa.
Alisema tabibu huyo aliomba rushwa kwa mgonjwa aliyekuwa na rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga .
Alisema awali mgonjwa huyo alibainika kuwa na tatizo la ngiri na madaktari walikuwa wamempatia rufaa ya kwenda kutibiwa hospitali ya mkoa.
"wakati wakijiandaa kutekeleza hilo alikutana na mtuhumiwa Joshua ambaye alimuhakikishia kuwa anauwezo wa kumfanyia upasuaji na ngepona na aliomba apewe fedha kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kazi hiyo"alisema Mwenda.
Alisema kutokana na hali hiyo mgonjwa huyo aliendelea kupata maumivu makali na hali ya kidonda kuwa mbaya zaidi kiasi kwamba mpaka utumbo kutoka nje na kusema mtuhumiwa amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Aidha alisema katika hatua nyinge wanamshikilia afisa mmoja wa TRA kwa kosa la kuomba na pokea rushwa ya shilingi laki tano kutoka kwa mfanyabishara mmoja wa mjini Sumbawanga ili amsaidie kupunguza kadirio ambalo alimwongezea katikati ya mwaka.
Alisema licha ya hilo wana washikiria viongozi watatu wa vyama vya ushirika mkoani humo kwa tuhuma za ubadilifu wa fedha za vikundi hivyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.