Mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU- mkoa wa Rukwa umewaagiza makatibu wa halmashauri zote nne za mkoa huo kutumia msaada wa kisheria ili kuwathibiti badhi ya waajiri wanaotuhumiwa kudhulumu haki na stahili za wafanyakazi wao
katibu wa TALGWU mkoa wa Rukwa, Sospeter Challo amezitaja baadhi ya haki na stahili wanazodhulumiwa wafanyakazi katika halmashauri za wilaya ya Sumbawanga, Nkasi, Kalambo na manispaa kuwa ni pamoja na kunyimwa masurufu ya uhamisho na kuelezea moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa chama hicho katika kuthibiti haki za watumishi wanapopata uhamisho haki zinazodaiwa kuminywa na baadhi ya waajiri
Mgeni rasmi katika mkutano huo wa TALGWU ngazi ya mkoa mkuu wa wilaya ya Sumbawanga dokta Halfany Haule ,amesema baadhi ya watumishi katika serikali za mitaa wanatuhumiwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kutaka kujinufaisha wenywewe.
Mkutano mkuu wa siku mbili wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa-TALGWU-mkoa wa Rukwa umehusisha pia mafunzo ya uelewa wa sheria mahali pa kazi
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.