Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa nchini kimeanzisha mfuko maalumu wa kuwainua kiuchumi wanawake watumishi wa serikali za mitaa ili kuwaepusha na mikopo kausha damu.
Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa taifa Christina Lyowa kupitia kikao cha kusikiliza kero za watumishi wa idara ya afya wilayani Kalambo mkoani Rukwa, amesema lengo ni kuwawezesha wanawake watumishi kijiimarisha kiuchumi kwa kuepuka mikopo mbayo imekuwa sehemu ya kudharirisha utu na taaluma yao.
Kaimu mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa TALGWU mkoani Rukwa Yustus Wandula ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa idara ya afya wilayani humo kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo ya serikali sambamba na kujiepusha na ukopaji wa fedha kwenye taasisi zisizo tambulika na serikali.
Viongozi wa chama hicho wamefanya ziara katika wilaya ya Kalambo na Sumbawanga huku lengo likiwa ni kusikiliza kero za watumishi kisha kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuzindua mfuko wa uwezeshaji wanawake watumishi kiuchumi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.