Wizara ya Afya kisiwani Zanzibar imetangaza wagonjwa saba wapya wa virusi vya corona .
Tangazo hilo linafanya idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona waliothibitishwa kisiwani Zanzibar kufikia 105 na jumla ya 306 nchini Tanzania.
Kulingana na taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari wagonjwa wote wapya ni raia wa Tanzania.
Aidha taarifa hiyo iliotiwa saini na waziri wa Afya kisiwani humo imesema kwamba wagonjwa 36 wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya dalili zao za mardhi ikiwemo homa, kikohozi, kifua kubana na kuumwa na kichwa kuisha.
Vile vile taarifa hiyo imesisitiza kwamba wagonjwa wote hao wameshauriwa kusalia katika nyumba zao kwa muda wa siku 14 huku wataalam wa afya wakiendelea kuwafuatilia kwa karibu kabla ya kuruhusiwa kurudi katika shughuli zao za kawaida.
Wakati huohuo serikali kupitia wizara ya Afya ,inaendelea kuwasisitiza wananchi ambao wana dalili za homa kali, kukohoa na kupiga chafya kujitokeza katika vituo vya Afya au kupiga simu nambari 190.
Vilevile vyombo vya habari vimetakiwa kupata taarifa za ugonjwa huo kutoka kwa wizara ya Afya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.