Serikali hapa nchini imethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona, kilichotokea alfajiri ya siku ya Jumanne tarehe 31 mwezi Machi mwaka 2020.
Mgonjwa huyo alifariki katika kituo cha matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila jijini Dar es Salaaam.
Marehemu ni mwanaume mtanzania mwenye miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.
Hapo jana Waziri wa afya Ummy Mwalimu alitangaza wagonjwa wapya watano wa virusi vya corona inayofikisha idadi ya wagonjwa kufikia 19.
Kwa mujibu wa taarifa ya waziri Ummy, wagonjwa hao wapya watano wote ni raia wa Tanzania.
Wagonjwa wawili ni kutoka visiwani Zanzibar na watatu kutoka Dar es Salaam.
"Kazi ya kufuatilia watu wote wa karibu waliokutana na wagonjwa hawa inaendelea (contact tracing). Aidha tunawataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhai ili kujikinga na ugonjwa huu," ameeleza Bi Mwalimu.
Taarifa ya wizara ya Afya ilibainisha kuwa kati ya wagonjwa hao wawili (mwanamke mwenye miaka 21 na mwanaume mwenye miaka 49) walikuwa wakifuatilia hali zao na watatu (mwanaume mwenye miaka 49) "alikutana na raia wa kigeni kutoka miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi."
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.