Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba ameikabidhi Kombe,Ng’ombe na seti moja ya jezi timu ya mpira wa miguu ya Mtapenda kutoka kata ya Mbuluma wilayani humo baada ya kuibuka na ushindi katika michezo ya ligi kuu ngazi ya wilaya ambayo ilikuwa ikiendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Kateka kata ya Matai na kushirikisha timu 32.
Awali akikabidhi zawadi kwa timu zilizofanya vizuri kwenye michezo hiyo mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Lazaro Komba ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujikita kwenye michezo ambayo itawawezesha kuimarisha afya na kuonesha vipaji vyao kwani michezo ni ajira.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29-2025 ili kuchagua viongozi wanao wataka kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla na kusisitiza kuwapuuza watu wanao shawishi vurugu na maandamano kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilayani humo Ndugu Ajuaye Kaduma, amesema michezo hiyo itakuwa endelevu na kwamba timu ya Mtapenda FC kutoka kata ya Mbuluma imeshika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa Kombe, Ng’ombe na seti moja ya jezi,Mshindi wa pili ilikuwa timu ya Maize Fc kutoka kata ya Mkali ambayo ilipata seti moja ya jezi na fedha shilingi elfu Hamsini (50,000/=) ikifuatiwa na timu White star kutoka kata Mkowe ambayo ilizawadiwa seti ya jezi na fedha shilingi elfu ishirini (20,000/=).
Michezo hiyo imedhaminiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kalambo pamoja na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU na kushirikisha timu 32 kutoka kata 23 za wilaya hiyo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.