Taasisi Ya Ukaguzi wa mbegu Za Mahindi Tanzania Tosci Imepiga Malafuku Wafanyabishara Wa Pembejeo Za Kilimo Nchini Kuuza Na Kusambaza Mbegu Ya Zam Seed Kutokana na mbegu Hizo Kutokuwa Na Ubora na Kusisitiza Kuchukua Hatua Kali Za kisheria dhidi ya Wafanyabiashara na makampuni ambao Watabainika Kuwauzia na Kuwasambazia wananchi pembejeo feki.
Katika Ukaguzi uliofanywa na Taaasisi hiyo Katika Mikoa Ya Rukwa na Katavi Wamebaini Baadhi Ya Wafanyabishara Kuuza Pembejeo feki na Kutoa aagizo kwa makampuni husika kuacha kusabaza mbegu kinyume na utaratibu.
Mkaguzi wa mbegu nyanda TOSCI nyanda za juu kusini Julias bwile, amesema wamefanya ukaguzi katika mikoa hiyo lengo likiwa ni kujiridhisha kama wafanyabishara wanafuata sheria na kanuni za uuzaji wa pembejeo hizo.
Amesema katika sehemu zote wamebaini baadhi ya wafanyabiashara kuuza pembejeo ambazo hazina chapa ya taasisi hiyo na kusema watu wote waliobainika kusambaza mbegu hizo kinyume na utaratibu watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Fred faida ambae ni mkaguzi wa tosk Tanzania amesema katika ukaguzi huo wamebaini mbegu ya Zam seed kuuzwa bila kuzingatia viwango na kusema wameisimaisha mbegu hiyo mpaka watakapojiridhisha zaidi.
Baaadhi Ya Wafanyabishara Mkoani Rukwa Wamesema Changamoto kubwa ni Wasambazaji kuto wapatia vyeti vya usambazazi Wa bidhaa Zao na kutaka kampuni kuzingatia sheria na kanunu zinazotolewa na mamlaka husika kabla ya mzigo kuwafikia kwenye maeneo husika.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.