Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi 87,000,000/= kisha kuanza ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Mkapa halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa vitakavyosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongeza hali ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
Ujenzi wa shule hiyo unajumuisha ujenzi wa matundu 6 ya vyoo ambao umefikia asilimia 98 ya ukamilishaji.
“Tunatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule,’’Alisema mkuu wa shule hiyo Thomas Ndunguru.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ametembelea shule hiyo kisha kuupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa usimamizi thabiti uliowezesha mradi huo kutekelezwa kwa viwango na kukamilika kwa wakati.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.