Umoja wa wasanii wilayani kalambom mkoani Rukwa umeungana na watu wengine mkoani humo katika zoezi la uchangiaji damu lililofanyika katika kituo cha afya Matai kwa lengo la kuwasaidia majeruhi walioungua moto uliosababishwa na kulipuka kwa roli la mafuta siku za hivi karibuni mkoani morogoro.
Wakiongea wakati wa zoezi la uchangiji damu lilioambatana na usafi wa mazingira, wasanii hao wamesema miongoni mwa madhara makubwa wanayopata watu pindi wanapota ajari ni pamoja na kupoteza damu nyingi hivyo kwa kuliona hilo wamelazimika kuchangia damu lengo likiwa ni kuwasaidia watu waliokuwa wameathirika na ajari ya moto mkoani morogoro.
“tufahamu kuwa mtu yeyote aliyeungua sehemu yoyote ya mwili, miongoni mwa madhara makubwa anayoyapata ni pamoja na kupoteza kiasi kikubwa cha maji mwilini (Dehydration) na kupungukiwa damu mwilini (Anaemia). Hivyo tunaomba watu wote wa Mkoa wa Rukwa kuchangia Damu kwa ajili ya wenzetu majeruhi wanaoendelea na matibabu’’walisema wasanii hayo.
Mwenyekiti wa umoja humo Ana Mwanga amesema licha ya kuchangia damu pia wameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika kituo cha afya Matai .
‘’licha ya kufika hapa kwa lengo la kutoa damu, pia tumeona ni vyema tukaitumia siku ya leo katika kufanya usafi ili kuyaweka safi mazingira ya kituo chetu cha afya.alisema Mwanga.
Mkuu wa mkoa Rukwa Joachim Wangabo amesema zoezi hilo litawajumuisha Waendesha Bodaboda na Bajaji,Madereva wa Magari, Vijana, Watumishi wa Serikali, Wanafunzi,Vyama za Siasa, Madhehebu ya Dini, Viongozi mbalimbali na wale wote wenye mapenzi mema na moyo wa kujitolea kwajili ya majeruhi hao.
Aidha Mh. Wangabo kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa anaungana na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Viongozi wa Mkoa huo, Familia za Marehemu, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Wapendwa wao. Na kumuomba Mwenyezi Mungu awape Moyo wa Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
“Mungu awape pumziko la milele waliopoteza uhai na awaponye Majeruhi wote wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro. ‘Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa Jina lake lihimidiwe’.” Alimalizia.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.