• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Vijiji 45 Kunufaika Na Mpango Wa TASAF Wilayani Kalambo,

Posted on: May 26th, 2021

Halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanza utekelezaji wa kuibua kaya masikini katika vijiji 45 ambavyo vilikuwa vimesalia katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo huku ikijidhatiti kuondoa wanufaika hewa kwa kuweka mfumo rafiki wa malipo ya njia ya simu za mkononi.

Katika kipindi cha kwanza, vijiji na mitaa 9,960 sawa na 70% vilifikiwa , ambapo jumla ya kaya milioni 1.36 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya milioni 1.1 zenye jumla ya watu milioni 5.4 ziliandikishwa kwenye masijala ya walengwa.

Hata hivyo katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, kilizinduliwa rasmi, februali 17-2020 huku kipindi cha pili awamu ya tatu ya TASAF (PSSN 11) kilianza kutekelezwa mwaka 2020 hadi mwaka 2023 ambapo wilaya 184 za Tanzania bara na visiwani ikiwemo Unguja na Pemba ziliingizwa kwenye mfumo huo.

Hata hivyo kwa wilaya ya Kalambo mpango huo umelenga kuvifikia vijiji 45 ambavyo vilikuwa vimesalia katika awamu iliyopita, ambapo Halmashauri imeunda timu za wasimamizi na wawezeshaji wa zoezi hilo katika vijiji hivyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Msongela Palela amebainisha kuwa zoezi la utambuzi wa kaya utafanywa na wanajamii kupitia mikutano ya vijij/Mitaa kwa usimamizi wa wawezeshaji kutoka kwenye mamlaka za maeneo husika.

Aidha Msongela alibainisha kuwa walengwa watakuwa ni kaya zinazoishi katika mazingira duni na hatarishi.

“Vigezo vya kaya za walengwa ni kaya ambazo zinakipato cha chini si cha uhakika ukilinganisha na kaya zingine katika kijiji au mtaa, pia zitaangaliwa Zaidi kaya ambazo hazimudu au hazina uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku pamoja na familia zenye makazi duni. Alisema Msongela’’

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa kunusuru Kaya masikini TASAF nchini Beatrice Shemdoe,alisema kipindi cha pili awamu ya Tatu ya Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF II) kinatekelezwa katika Halmashauri 184 za Tanzania bara na visiwani na kubainisha kuwa kipindi hiki kitafikia zaidi ya wananchi milioni moja nchini kote.

“Mkazo mkubwa katika kipindi chapili umewekwa katika kuziwezesha kaya masikini ili kuziongezea kipato’’ alisema Shemdowe.

Alisema walengwa watakao tambuliwa na kuandikishwa katika kipindi cha pili ni kaya zinazoishi katika hali duni kwenye vijiji, mitaa na shehia na kwamba wanufaika ndani ya kaya watakuwa ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanao hudhuria kliniki.

Mkuu wa wilaya hiyo Kalorius Misungwi aliwasisitiza watendaji kuwa waadilifu wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo na kuwasisitiza kufanya kazi kwa bidii kwa malengo ya kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi ukiwemo ule wa viwanda ambayo ni ajenda muhimu ya serikali.

“Nitoe ushauri kwa viongozi wenzangu, tunapofanya ziara zetu za kikazi katika maeneo yetu tutenge muda wa kuongea na walengwa na kuwahamasisha kuanzisha miradi ya ujasiriamali ili kukuza vipato vya kaya zao na kuwa na akiba ya kujikimu ili hata pale ruzuku inapochelewa au kusitishwa wawe wamejiwekea misingi bora. Alisema Misungwi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.