Wanufaka wa mradi wa TASAF wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vitakavyo wawezesha kukuza uchumi wa kaya kwa kuanzisha miradi ya pamoja na kupata mikopo itakayo wawezesha kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa TASAF wilayani humo Mariam Kimashi wakati wa kampeni ya uundwaji wa vikundi kwenye vijiji vya kata za Matai na Lyowa. Ambapo amesema kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa vikundi, Halmashauri imeanzisha mpango wa kuwaunganisha wanufaika kwenye vikundi na kwamba wanatarajia kuunda vikundi 200 ambapo kila kikundi kitakuwa na wanufaika 15.
‘’lengo la serikali ni kuwaweka pamoja wanakikundi ili kuongeza uchumi wa kaya na kwamba endapo kikundi kitafanya vizuri na kuwa na uwezo basi TASAF itakipatia ruzuku ya uzalishaji ili kuifanya kaya kujikwamua kiuchumi’’alisema Kimashi
Hata hivyo baadhi ya wanufaika wa TASAF wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuwawezesha kifedha na kwamba kuanzishwa kwa vikundi hivyo kutaenda kuwaondolea adha ya kuwa tegemezi katika jamii.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.