• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Viongozi Wa Dini Rukwa Watahadharisha Fujo Siku Ya Uchaguzi Huku Wakiliombea Taifa

Posted on: October 27th, 2020


Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Rukwa kupitia Kamati ya Amani ya Mkoa huo wamewatahadharisha wananchi hasa kundi la vijana kuachana na fikra za kuanzisha ama kuchochea fujo katika siku ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika kesho tarehe 28.10.2020.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti wameyasema maneno hayo katika siku ya maalum iliyoandaliwa na Kamati hiyo ya Amani mkoani humo ili kuliombea taifa amani na kuuombea uchaguzi huo ufanyike kwa utulivu huku wakiwasihi wananchi kushiriki katika uchaguzi huo na kuondoka katika kituo cha uchaguzi mara tu baada ya kumaliza zoezi la kumchagua wanayemwona anafaa kuwaongoza kuanzia ngazi ya Kata, Jimbo na Nchi.

Wakati akitoa nasaha zake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Rukwa, Askofu Ambele Mwaipopo wa Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa aliwaomba wananchi kuwachagua viongozi watakao ipeleka nchi ya Tanzania inapotakiwa kwenda na sio viongozi wanaoleta mizaha katika maendeleo ya nchi.

“Kwahiyo siku hiyo tupige kura tuwachague viongozi ambao wanatokana na kiti cha enzi cha Mungu mwenyewe, Mungu ameshajichagulia viongozi katika taifa hili, sisi tutathibitisha kwa kura zetu na Mungu apate kutukuzwa na abaki katika nchi ya Tanzania ipate kusonga mbele,” Alisema.

Naye Kiongozi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Mkoani Rukwa Sheikh Rashid Akilimali alisema kuwa vijana wa hivileo hawajawahi kushuhudia kutoweka kwa amani na kusahau kuwa kuna nchi za jirani ambazo waliwahi kushuhudia kutoweka kwa amani y ana matokeo yake walikimbilia nchini kwetu Tanzania kwaajili ya hifadhi na hivyo kuiomba serikali kuhakikisha vijana watakaosababisha fujo warudishwe katika mstari.

“Tarehe 28 tukapige kura ndio wito wangu, tuwachague viongozi ambao tutaona watatuletea maendeleo, tukawachague na mkuu wa mkoa anasema yule ambaye anaona hajakaa sawa kiroho akaenda kimwili tutamrudisha, mrudisheni kikwelikweli, asituvunjie amani yetu, mrudisheni, awe katika mstari barabara, tukapige kura asubuhi tumchague kiongozi tunayemtaka, kisha baada yah apo turudini kwenye makazi yetu,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa rukwa mh. Joachim Wangabo aliyehudhuria katika dua hiyo maalum amesema kuwa kuna matayarisho ya kimwili na kiroho katika kuliendea zoezi la uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa matayarisho ya kimwili yote yamekamilika ikiwemo Tume ya uchaguzi ya Taifa Pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kujipanga vyema kukabiliana na wale ambao watakuwa wamekengeuka ambao hawataki kufuata maswala hayo ya kimwili.

“ lakini tupo hapa kuwaombea hao na kuiombea nchi yetu amani, sina shaka kabisa, Mwenyezi mungu amekuwa akitusikia, Ametusikia kwenye janga lile la Corona, sasa na hili pia atatusikia, imeandikwa kwenye maandiko matakatifu kwamba wakutanapo wawili wakimuomba yeye yupo na hapa tupo Zaidi ya wawili, tuko wengi viongozi hawa waliopo hap ani wawakili tu wa waumini wote,” Alisema.

Maombi hayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari kizwite ikiwa ni kutimiza azma ya Kamati ya Amani mkoa kuliombea taifa kuwa na uchaguzi wa amani

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.