Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Rukwa wametoa wito kwa waumini wao juu kuwapuuza watu wanao shawishi kupitia mitandao ya kijamii ili kufanya vurugu na maandamano wakati wa uchaguzi mkuu na badala yake wajitokeze kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi wanao wataka kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Wameyabainisha hayo wakati wa ibada ya Jumapili na kusisitiza waumini kuendelea kuombea uchaguzi mkuu ili uweze kufanyika kwa amani na utulivu na kubainisha kuwa wao na serikali ni kituo kimoja hivyo ni jukumu lao kuhakikisha amani na upendo wakati wa uchaguzi vinatamalaki.
Awali akisoma walaka uliotolewa na kanisa la K.K.T Mwinjilisti Lupakisyo Mwakyolile kutoka usharika wa Matai wilayani humo, amesema kila muumini ana wajibu wa kuliombea Taifa na uchaguzi mkuu ikiwa ni Pamoja na kujitokeza kupiga kura kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mapema akiongea kupitia mahubiri ,mwangalizi wa kanisa la TAG jimbo la Rukwa Magharibi mchungaji Deodatus Mwanisawa ametumia fursa hiyo kuwataka waumini kuwa sehemu ya kuhamasisha amani,upendo na utulivu katika Taifa kwa kuwapuuza watu wanao chochea vurugu na maandamano kupitia mitandao ya kijamii.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.