Waamini wa madhehebu mbalimbali ya kidini mkoani Rukwa wamewapongeza wachungaji wa madhehebu mbalimbali ya kidini mkoani Rukwa kwa kufanya maamuzi ya kufungua shughuli za ibaada licha ya baadhi ya makanisa kutofungua shughuli hizo kwa kuhofia ugonjwa wa Corona.
Katika nyakati tofauti waamini wa madhehebu hayo wamebainisha kuwa kipindi cha CIVD 19 viongozi wao waliungana na serikali katika kupinga na kukemea uwepo wa ugonjwa huo kwa kuweka utaratibu wa kupunguza muda wa ibada lengo likiwa ni kuwawezesha kuendelea kupata neno la mungu.
Wamesema kitendo hicho kilisaidia kuongeza Imani yao mara dufu na kusema mpaka sasa wanaendelea na ibada kama ilivyokuwa awali kutokana na mwenyezi mungu kutenda miujiza ya kutokomeza ugonjwa wa corona.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.