• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Viongozi Wapya Wa Serikali Za Mitaa Wafundwa Baada Ya Kuapishwa.

Posted on: December 2nd, 2019

Viongozi wapya 2,766 wa vijiji na vitongoji walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika tarehe 24.11.2019 katika wilaya ya Kalambo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatatua kero na malalamiko ya wananchi wanaowahudumia katika vijiji na vitongoji ili kupunguza msongamano wa wananchi wanaohitaji kutatuliwa kero zao katika ngazi ya wilaya na mkoa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo muda mfupi baada ya viongozi hao kula kiapo mbele yake na mbele hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kalambo ambapo wenyeviti wa vijiji na vitongoji kutoka katika kata 10 za tarafa ya Matai wilayani humo walishiriki katika kiapo hicho.

“Katika ngazi hiyo ya vijiji, vitongoji na mitaa, wenyeviti wa maeneo hayo mimi nikipata mtu anatoka kwenye vijiji vyenu analalamika kwa jambo ambalo ni dogo sana, nitakuita. Utapata usumbufu wa kuja Sumbawanga, uhesabu kuwa utatumia gharama zako kuja na kurudi kutoka kule kwenye kijiji chako. Nitakusumbua kwasababu wewe hutaki kusumbuka nikilipata tu nitakusumbua, kwahiyo nendeni mkatatue kero za wananchi katika ngazi zenu, yako mambo mengi mtusaidie sio kila kitu mkuu wa mkoa, kila kitu mkuu wa Wilaya na wengine wanakwenda wanaandika mpaka kwa Rais,”Alisisitiza.

Aidha amewataka viongozi hao kuwatumikia wananchi wote bila ya kujali vyama vyao vya kisiasa, dini wala kabila na kuwataka katika utekelezaji huo kuwa shirikisha kwani wasipofanya hivyo wananchi watashindwa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo jambo litakalorudisha nyuma juhudi za mkoa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma stahiki na kwa wakati.

“Mambo ambayo mnapaswa kwenda kuyasimamia katika maeneo yenu kuwashirikisha wananchi katika kupanga maendeleo, sio unakurupuka tu unasema mimi nataka hiki kifanyike bila ya kuwashirikisha wananchi , lazima wapange waamue wao wenyewe na wakishaamua wao wenyewe watashiriki katika kutekeleza lakini pia watasimamia kulinda yale maamuzi yao na hiyo ndio demokrasia na hili ndilo mkalifanye kule, viongozi wengine wakishachaguliwa kama hivi wanakuwa miungu watu, hatupendi kuona miungu watu kwenye vijiji vitongoji na mitaa,” Alisema.

Na katika kuhakikisha viongozi hao wanatekeleza majukumu yao bila ya visingizio amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nne za mkoa huo kuwapatia mafunzo viongozi hao wapya pamoja na wale ambao ni muhula wao wa pili au zaidi jambao litakalo wasaidia kutekeleza majukumu yao kwa Mujibu wa Sera za Kisekta, Mikakati ya Kisekta, Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu zinazosimamia Sekta husika.

Wakati akitoa muhtasari wa taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa mratibu wa uchaguzi mkoa Albinus Mgonya alisema kuwa mitaa 165 iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga imechukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ni sawa na asilimia 100 wakati katika ngazi ya vijiji CCM imechukua vijiji 336 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikichukua vijiji 2 kati ya vijiji 339 vya mkoa wa Rukwa.

“Vitongoji vilivyoshiriki katika uchaguzi ni 1,816 na kwa nafasi ya vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepata nafasi 1,807 sawa na asilimia 99.4 Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimepata nafasi za wenyeviti wa vitongoji 8 sawa na asilimia 0.6. kwa faida ya wadau waliopo hapa nafasi hizi 8 mgawanyo wake ni kama ifuatavyo, Sumbawanga Manispaa nafasi 1, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga nafasi 1 na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi nafasi 6,” Alimalizia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone wakati akitoa neno la shukurani aliwataka viongozi hao wapya kuhakikisha wanawapatia elimu ya kutosha wananchi wanaowaongoza juu ya kutatua kero na malalamiko katika ngazi hizo zao na sio kumshawishi mwananchi afike ngazi mkoa.

“Hawa viongozi wetu wanatumia mkoa na taifa, hebu ifike mahali tutoe elimu kwa wananchi wetu, kabla hajafika huko angalau akifika kule ionekane sisi sote tunasapoti kwamba kwa tatizo lako hili ni vyema ukafika kwa mkuu wa mkoa lakini sio tu unaamka tu na masimu yako unamuhangaisha mzee wa watu anashindwa kufanya kazi za watu,”Alisema.

Maeneo yaliyofanya uchaguzi katika mkoa wa Rukwa ni vijiji 67, vitongoji 348, mitaa 9 na wananchi walioshiriki kupiga kura ni 118,887 huku zoezi hilo la uchaguzi likiwa limefanyika katika hali ya amani na utulivu.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.