Wabunge nchini Tanzania wataanza kutumia tablet kwa ajili ya kazi za bunge, huku bunge hilo likiondokana na matumizi ya karatasi.
Wabunge walikabidhiwa vifaa hivyo Jumatatu kabla ya kuanza kwa vikao Jumanne mchana katika mji mkuu wa nchi hiyo Dodoma.
Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhifadhi pesa ambazo serikali imekuwa ikizitumia kuchapisha na kunakili nyaraka za serikali.
" Hata hivyo tumeziomba wizara husika kuja na baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuweka rekodi yake. Kwa mfano kwa matumizi katika maktaba," alisema.
Bwana Kigaigai anasema imekuwa ikichapisha nakala 500 za nyaraka za kutumiwa katika shughuli za bunge kwa siku lakini kwa sasa zitakuwa chini ya nakala 10.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wabunge wote leo wameingia bungeni na Tablet.
Spika wa bunge hilo Job Ndugai amezitaka taasisi nyingine nchini Tanzania kuiga mfano wa bunge kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kupunguza matumizi ya karatasi.
Anatarajia hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama ya kuchapisha kutoka shilingi bilioni 1.2 sawa na $519,000 hadi shilingi milioni 200.
Bunge limenunua takriban tableti 450 zenye thamani ya shilingi milioni 900 sawa na $389,000.
Bunge la Tanzania limekuwa ni bunge la hivi karibuni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kutumia teknolojia katika kuimarisha utendaji wa haraka na kupunguza matumizi.
Katika nchi jirani ya Kenya wabunge walipewa iPad mapema mwaka huu katika hatua iliyotarajiwa kunusuru shilingi milioni 15 sawa na dola $150,000 ambazo zimekuwa zikitumiwa kuchapisha nakala za shughuli za bunge.
Uganda ilitoa iPad kwa wabunge nchini humo mwaka 2013.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.