Wafanya biashara wa mifugo ya Ng’ombe wilayani kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuboresha mazingira ya mnada wa mkoe ili yaendane na bishara husika kutokana na maeneo hayo kuwa na ukosefu wa huduma ya choo tangia kuanzishwa kwake na hivyo kuwa na hofu ya kupata magonjwa yamilipukoikiwemo kipindupindu.
Wilaya ya kalambo ina jumla ya minada nane ya mifugo na ng’ombe wapatao lakimoja na elfu sita ,ambapo kutokana na hali hiyo watu kutoka sehemu mbalimbali hufika katika maeneo hayo kwa lengo la kufanya bishara ya mifugo.
Wafanyabishara wa mifugo wilayani humo wamesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa miundombinu kuziguka soko hilo ambalo linajumusha wafanyabishara kutoka sehemu mbalimbali
Pita Chambanenje mfanyabishara na mkazi wa kijiji cha mkoe alisema serikali haina budi kuwangaalia kwa jicho la tatu hususani katika kuweka huduma muhimu ikiwemo choo kwa lengo la kuepukana magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.
Jelly mkombozi-mfanyabishara alisema licha ya hilo katika maeneo hayo barabara imekuwa chanagamoto kwani wamekuwa wakishindwa kupitisha magari na kusema chanagamoto kubwa imekuwa ikijitokeza wakati masika .
Mkurugez mtendaji wa halmashauri hiyo Msongera Palela amesema serikali imejipanga kuboresha miundombinu yote kwenye maeneo hayo ikiwemo kujenga vyoo vya kudumu.
‘’Kama halmashauri tunamkakati wa kujenga wigo katika maeneo haya lengon likiwa ni kuwasaidia wafanyabishara kuondokana na adha ya kuibiwa mifugo yao na pia hii itasaidia kwa kiasi kikubwa wafanyabishara kufanya biashara zao kwa uhuru zaidi’alisema msongera
Aidha amesema licha ya hilo halmashauri inamkakati wa kuweka huduma ya choo kwenye maeneo hayo na kuwataka kuendeleab kufanya usafi kilawakati.
Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura aliwataka wafanyabishara kulipa kodi kwa kulipia fedha za vitambulisho vya ujasilia mali.
‘’ kila mfanya bishaara anawajibu wa kulipa kodi,endapo mkilipia vitambulisho hivyo kila mtu atakuwa na uhuri wa kufanya bishara popote hata ukienda mbeya utafanya biashara zako bila bugudha’’.alisema Binyura
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.