SERIKALI imeanzisha kampeni maalumu ya kupambana na magonjwa ya mifugo kwa kusambaza dawa katika majosho yote ikiwa ni jitihada za kuwasaidia wafugaji ili kuondokana na changamoto ya kufa kwa mifugo yao.
Ofisa mifugo mfawawidhi wa kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kanda ya kusini magharibi Dkt Kaini Kamwela,alisema kuwa huo ni mkakati wa serikali katika kuhakikisha wafugaji wanafuga mifugo yao kitaalamu na kuondokana na adha ya kufa kwa mifugo yao.
Alisema kwa muda mrefu wafugaji wamekuwa wakikutana na chanagamoto ya kushindwa kuongesha mifugo kutokana na ukosefu wa dawa pamoja na gharama ya kuongeshea mifugo kuwa kubwa.
Alisema kwa kutambua hilo serikali imepunguza gharama za kuongeshea mifugo kwa asilimia mia moja.
Aliyasema hayo mara baada ya kutembelea josho la kuogeshea mifugo lililopo katika kijiji cha Kate wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Baadhi ya wafugaji katika kijiji hicho waliipongeza serikali kwa jitihada hizo na kusema kuwa awali walikuwa wakiogesha mifugo kwa bei kubwa na hivyo kusababisha kushindwa kumudu gharama sambamba na matibabu kuwa bei juu.
"tunaishukuru sana serikali kwa jitihada zake katika kuwapatia dawa za mifugo pamoja na kuongeza idadi ya mashojo kwani hatua hiyo itawawezesha kuondokana na changamoto ya kufa kwa mifugo yetu’’ walisema wafugaji hao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.