Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza kuongezeka kwa wagonjwa 14 wapya wa corona .
Wagonjwa wote 14 ni raia wa Tanzania. Kufikia sasa watu 46 wameambukizwa virusi vya corona.
Watu 13 kati ya walioambukizwa viruri vya corona wapo jijini Dar es Salaam huku na mwingine mmoja kutokea mjini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya Jumatatu asubuhi wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
''Ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu nao unaendelea'' ilisema taarifa hiyo.
Maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa nchini Tanzania ni Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Mwanza.
Hapo jana mamlaka nchini Tanzania zilitangaza marufuku ya ndege za abiria kutua nchini humo.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa siku ya Jumapili na mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo (TCAA) ndege za mizigo pekee ndizo ambazo zitaruhusiwa kutua.
"Rubani na wahudumu wa ndege hizo watatakiwa kukaa kwenye karantini katika maeneo yaliyotengwa na serikali kwa gharama zao binafsi," ilisema tangazo hilo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.