Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Msongela Palela kufuatilia na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahudumu wa afya ambao wamekuwa wakitoroka muda wa kazi kwenye vituo vyao na kupelekea malalamiko kutoka kwa wagonjwa kutokana na kukosa huduma kwa muda unaostahili.
Ameyasema hayo wakati akisikiliza kero mbalimbali za wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliojumuisha vijiji nane kutoka kata za Lyowa na Matai wilayani kalambo mkoani hapa na kuwasisitiza wahudumu wa afya kufanya kazi kwa bidii na kuondokana na vitendo vya utoro kwenye maeoneo yao ya kazi kwa lengo la kuondokana na malalamiko yasiyo kuwa ya lazima kutoka kwa wananchi.
‘‘Hili nalikemea lisitokee tena na sasa naanzisha utaratibu wa kukagua nyakati za usiku na ambaye nitakuta hayupo nitamchukulia hatua kwani atakuwa amevunja sheria.’’ Alisema Binyura.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Efraim Moses Mwalemba amewataka madiwani kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji katika kukusanya mapato ambayo yatasaidia kuendeleza shughuli za maendeleo.
‘’Waheshimiwa madiwani ndio wenye jukumu la kukusanya mapato wakishirikiana na watendaji wa vijiji na kata kwenye maeneo yao husika kwani fedha hizi huwa zinatumika katika shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo kuendeleza miradi ya Serikali, kulipa posho za madiwani na mambo mengine yahusuyo usitawi wa Halmashauri.’’alisema Moses
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.