Wananchi wilayani Kalambo wametakiwa kuziepuka taasisi za kifedha zisizokuwa na usajili kwa kuacha kuchukua mikopo sambamba na kutoa taarifa za uwepo wa taasisi hizo ili ziweze kufungiwa na wamiliki kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hayo yamebainishwa na afisa mkuu wa usimamizi wa fedha kutoka wizara ya fedha Salimu Kimaro wakati wa utoaji elimu kwa wajasiamali wadogo wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kusisitiza wananchi kuwa sehemu ya kuwafichua watu wanao kopesha fedha mitaani kinyume na utaratibu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na biashara zao kufungiwa.
Aidha, amezitaka taaisisi zinazotoa fedha kuhakikisha zinatoa mikataba inayaoeleweka kwa wananchi wakati wa kutoa mikopo na kusisitiza kuzifungia taasisi zote ambazo zitabainika kutoa huduma za kifedha bila kusajiliwa.
Baadhi ya wajasiliamali wadogo wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu wa kutoa elimu hiyo na kwamba itawawezesha kuondokana na mikopo kausha damu ikiwa ni pamoja na kuwatambua watu wanaopaswa kutoa mikopo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.