Wajasiriamali wadogo wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuweka nembo ya shirika la viwango Tanzania (TBS) ili ziweze kutambulika na kushindanishwa kwenye masoko ya nchi za Jirani ikiwemo Kongo na Zambia.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo Ndugu Vitus Nandi wakati wa maonyesho ya wafanyabiashara saba saba ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika katika kijiji cha Mikonko na kusisitiza wajasiriamali kuzingatia kanuni bora za usindikaji wa bidhaa zao kwa kuzingatia viwango vya shirika la Tanzania (TBS).
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo katika maeneo hayo wametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ambayo itawawezesha kuimarisha biashara zao na kuziuza katika nchi za Jirani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.